Maandalizi ya kuweka marumaru: Kazi za awali za sehemu ya tano katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimeanza.

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika mradi wa kuweka marumaru kwenye haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wameanza kazi za awali katika sehemu ya tano na ya mwisho, baada ya kusimama kwa siku kadhaa kwa ajili ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, sehemu hiyo ni upande wa kusini baina ya mlango wa Kibla na mlango wa Imamu Hassan (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, amesema kua: “Hakika kazi za maandalizi ni sehemu muhimu katika mradi huu, kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimechukua jukumu la kufanya kazi hiyo, tangu mradi huu ulipo anza wamekua washirika wetu katika utendaji, kutokana na uzowefu wao katika kazi hizi”.

Akaongeza kua: “Kazi za awali ni pamoja na:

  • - Kutoa marumaru za zamani.
  • - Kutoa zege la zamani na kurekebisha sehemu zilizo haribika.
  • - Kuziba sehemu zilizo pasuka kwa kutumia vifaa maalum.
  • - Kuweka zege maalum lenye viwango maalum vinavyo iwezesha kushikana vizuri na ardhi ya zamani pamoja na kuzuwia unyevunyevu.
  • - Kutengeneza tabaka la chuma chini ya zege.
  • - Kuweka mitandao ya maji, mawasiliano, zima moto, tahadhari na kuiunganisha na ukumbi wa haram pamoja na mifumo mikuu ya Atabatu Abbasiyya”.

Akasisitiza kua: “Kazi zinaenda kama zilivyo pangwa pamoja na kuhitaji umakini mkubwa katika utendaji wake, hasa wakati wa kuunganisha mitandao ya huduma katika mifumo yake”.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni mradi unao kamilisha miradi iliyo tangulia, mradi huu umeanza kutekelezwa kwa sababu ya kuharibika kwa marumaru za zamani kutokana na ukongwe wake, kwani zilikua na zaidi ya miaka (50), ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kufanya mradi huu kwa ajili ya kuongeza uzuri wa muonekano wa sehemu hii tukufu, kwa namna ambayo itatia amani na furaha katika nafsi za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: