Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya zimepata nafasi za mwanzo katika kutekeleza kanuni za (RDA)…

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya zimefanikiwa kufuata kanuni za (RDA) ambazo ni kanuni za kisasa kabisa zinazo tumika katika maktaba za kimataifa na imepata nafasi za mwanzo katika utekelezaji wa kanuni hizo.

Hayo yamesemwa katika mkutano wa nne (Ifla) unao husisha maktaba zilizopo katika nchi za kiarabu uliofanyika hivi karibuni katika falme za kiarabu, katika mkutano huo Dokta Muhammad Fat-hi Abdulhaadi aliwasilisha mada ya kitafiti chini ya anuani isemayo: (Athari ya uwelewa na maarifa ya namba katika utaratibu wa kazi za maktaba na vituo vya elimu za kiarabu), kupitia mada hiyo akatoa maelezo ya kitafiti na akataja maktaba za kiarabu zinazo fuata kanuni za (RDA) na zilizo fanya vizuri, miongoni mwa maktaba hizo ni Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua Maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu inajifunza kila jambo jipya la kielimu kuhusu maktaba na kulifanyia kazi, imejifundisha mambo mengi na kupata uzowefu mkubwa ndani ya muda mfupi, wala jambo hilo sio mzigo kwake, inafanya kila kitu kwa faida yake na faida ya maktaba za Iraq, katika hilo imepiga hatua kubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: