Miongoni mwa machapisho yake ya kiuhakiki: Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimetoa kitabu cha (Mustadrak Dhariáh).

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa vitabu vyake kwa kifikra, kimaarifa na kiuhakiki, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimezindua kitabu cha (Mustadrak Dhariáh) kilicho andikwa na mhakiki Ahmadi Majidi Hilliy, na akakitangaza pembezoni mwa kongamano la kielimu liitwalo (Alammah Shekh Aghaa Buzruk Twaharani na athari yake katika kuhuisha turathi za kiislamu), lililo fanywa na kitengo hicho kabla ya siku chache.

Kitabu hicho kimepitiwa na kuwekwa faharasi na kituo cha thurathi za Najafu, mwandishi ameweka maelezo ambayo hayakuandikwa na Shekh Aghaa Burzuk Twaharani katika kitabu cha (Dhariáh) hadi mwaka wa kufa kwake (1389h), ametaja pia nakala za idhini za Mustadrak, na sehemu vilipo vitabu na idhini hizo, akataja na tarehe ya kuandikwa kwake na baadhi ya mambo yaliyomo.

Vilevile ametaja nakala ya kwanza na masahihisho yake, akianza na kutaja historia fupi ya Shekh Twaharani (q.s), na akaandika mambo yaliyo msukuma kuandika kitabu cha (Dhariáh) na changamoto alizo pitia wakati wa kuandika kitabu hicho.

Fahamu kua kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimepiga hatua kubwa katika uandishi na uhakiki wa vitabu vya zamani, vyenye turathi za kiislamu kwa ujumla hususan turathi za kishia.

Kwa anayetaka kukiona aingie kwenye mtandao huu: http://www.mk.iq/releases.php ukitaka kupata kitabu hicho pamoja na vitabu vingine tembelea duka la vitabu lililopo mkabala na mlango wa Kibla wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: