Mradi wa kiongozi wa wasomaji umefungua milango ya kusajili wasomi wa Quráni wanaopenda kushiriki awamu ya tano.

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa imetangaza kufanyika kwa awamu ya tano ya mradi huo, nao ni miongoni mwa miradi ya Quráni iliyo chini ya Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kusajili wasomi wanaopenda kushiriki katika mradi huo.

Kamati imesema kua usajili unaendelea hadi (1 Mei 2019m) chini ya masharti yafuatayo:

  • 1- Maombi yanafanyika kwa njia ya mtandao peke yake, nao ni: https://t.me/AmeerAlquraa5
  • 2- Kwa ajili ya kurahisisha ushiriki, mwaka huu kamati imeamua kuwe na mtihani wa majaribio utakao fanyika kwa utaratibu ufuatao:
  • - Mtu anayetaka kushiriki atume usomaji wake wa lahaja (mahadhi) ya (kiiraq au kimisri) wa dakika moja na nusu au dakika mbili, katika usomaji wake azingatie Qaraar na Jawabu.
  • - Usomaji urekodiwe kwa kutumia video, mwanzoni mwa video hiyo ataje majina yake matatu na mkoa anaotoka, video isiyokua na hayo haitakubaliwa.
  • - Video itumwe pamoja na nakala ya maandishi inayotaja mambo yafuatayo:
  • 1- Majina matatu na laqabu.
  • 2- Tarehe ya kuzaliwa (siku – mwezi – na mwaka), umri usiwe zaidi ya miaka (17), awe amezaliwa baada ya (1 – 7 – 2002) tofauti na hivyo maombi hayatakubaliwa.
  • 3- Jina la mkoa, wilaya na tarafa.
  • 4- Namba za simu za mlezi wake, atatakiwa kumdhamini baada ya kukubaliwa kwake.
  • 5- Namba ya simu ya mwalimu wake, naye anatakiwa awe mdhamini wake baada ya kukubaliwa.
  • 6- Namba yake ya simu.

Mambo muhimu:

  • 1- Msomoji anatakiwa kuomba ushauri kwa mtu anaye mzidi, katika kuchagua aina ya usomaji na namna ya kutekeleza masharti yanayo takiwa, kuchagua usomaji usiotakiwa kunaweza kusababisha kukosa nafasi ya kuendelea katika mradi (baada ya kuchaguliwa kwa mara ya pili na walimu wa mradi).
  • 2- Mtu yeyote atakaye tuma taarifa zake mara mbili hazita kubaliwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: