Matawi tofauti ya Atabatu Abbasiyya tukufu yameshiriki katika maonyesho haya, kila moja likiwa na bidhaa zake, matawi yaliyo shiriki ni:
- 1- Vitalu vya Alkafeel: wameonyesha bidhaa mbalimbali kutoka kwenye vitalu pamoja na asali.
- 2- Shirika la uchumi Alkafeel: limeonyesha bidhaa mbalimbali za wanyama na kilimo na zinginezo.
- 3- Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud: limeonyesha bidhaa wanazo tengeneza kuanzia madawa, mbolea na kinga za maradhi mbalimbali ya mimea.
- 4- Kitengo cha miradi ya kihandisi: kimeonyesha miradi kiliyo fanya.
- 5- Makumbusho ya Alkafeel na vifaa na nakala kale: wameonyesha mambo mbalimbali.
- 6- Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji: kimeonyesha misaada mbalimbali ya kibinaadamu waliyo toa pamoja na picha za mashahidi wake.
- 7- Kitengo cha habari na utamaduni: kimeonyesha machapisho mbalimbali yaliyo tolewa na kitengo hicho.
- 8- Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu: kimeonyesha machapisho yake pamoja na picha zilizo tengenezwa na kituo cha turathi za Karbala ambacho kipo chini yake.
- 9- Hema la mafunzo ya huduma ya kwanza.
Matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yamefanyia kazi kauli ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) yasemayo: (Miradi yetu inachochea uwezo wa wairaq) wameifanya kua kauli mbiu yao, wameonyesha bidhaa za aina tofauti, kila bidhaa inamchango mkubwa katika kuboresha huduma za Ataba, pia ni kielelezo cha kazi nzuri inayo fanywa ya kujitegemea katika sekta mbalimbali za kiviwanda na upande wa kilimo pamoja na vitu vingine.