Maahadi ya Quráni inajadili uboreshaji wa selebasi ya somo la hukufu za usomaji wa Quráni.

Maoni katika picha
Selebasi ya somo la hukumu za usomaji wa Quráni inamapungufu mengi, kwa namna ambayo inaweka ugumu katika kufikisha elimu kwa usahihi, jambo hili limeifanya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la Najafu kuandaa warsha hii kwa anuani isemayo (Kuboresha selebasi ya somo la hukumu za usomaji) na kualika jopo la walimu wa hukumu za usomaji wa Quráni.

Wametaja mapungufu makubwa katika ufundishai wa hukumu za usomaji na namna ya kuyaondoa, pamoja na kuboresha selebasi kwa ujumla, sambamba na kuzingatia mahitaji ya kijamii na viwango vya wanafunzi wa Quráni, na vifaa vinavyo weza kutumiwa katika ufundishaji, sambamba na namna ya kunufaika na maendeleo ya kielimu ya sasa katika sekta ya ufundishaji.

Nadwa ilikua na mada nyingi, kama zikifanyiwa kazi tunaweza kupata selebasi bora zaidi inayo endana na elimu za kisasa, miongoni mwa vitu muhimu tulivyo kubaliana katika warsha hii ni kuainisha mada zitakazo fundishwa katika kila kozi, pamoja na kuainisha umri kusudiwa kwa kila mada (Umri mdogo, vijana, watu wazima na wazee) kila mada inapangwa kulingana na kiwango cha elimu ya walengwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: