(Misingi ya maisha yenye mafanikio) ni program ya kimalezi inayo ratibiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa wanafunzi wa shule.

Maoni katika picha
Kitengo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika utaratibu wa kuongeza uwelewa kwa wanafunzi wa ngazi zote, kimeanzisha program nyingi chini ya mikakati ya shule na kusimamiwa na wataalamu walio bobea, miongoni mwa program hizo ni hii ya (Misingi ya maisha yenye mafanikio) ambayo inalenga wanafunzi wa viwango tofauti na rika tofauti, baada ya kuwasiliana na idara za shule na ofisi ya malezi ya mkoa, hualikwa katika makao makuu ya kituo na program huendelea kwa mwaka mzima.

Kwa mujibu wa maelezo ya mmoja wa wasimamizi wa program hii inalenga: kuongeza uwelewa wa wanafunzi wa mazingira ya nyumbani na shuleni, kuwafundisha hatua za umri wanaopitia kinafsi na kijamii, pamoja na mahitaji ya kila hatua katika umri na namna ya kuamiliana na watu wengine, sambamba na kuangalia mafundisho ya sharia za kiislamu, kwa ajili ya kujenga mazingira yanayo faa kwa wanafunzi, na kuwafanya waishi kwa Amani na utulivu.

Program hii inahusisha warsha na mihadhara tofauti, inayo zungumzia maadili mema na kuwatahadharisha na hatari wanazo weza kukutana nazo, ikiwa ni pamoja na kuwafahamisha hatua bora zenye mafanikio katika maisha yao na namna ya kuwa na fikra chanya, misingi ya malezi ya watoto, kukata tamaa na mengineyo mengi.

Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia, ofisi zake zipo katika jengo la Swidiiqah Twaahirah kwenye mtaa wa Mulhaq mkoa mtukufu wa Karbala, kimebobea katika mambo ya familia, kilianzishwa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kifamilia hapa Iraq na kusaidia utatuzi wa changamoto za kijamii, pamoja na kusaidia upatikanaji wa utulivu wa nafsi kwa wanafamilia, hutoa mafunzo ya kinafsi kwa watu wote wa familia, na hufuatilia mafunzo yao chini ya utaratibu maalum na kwa kutumia watu walio bobea katika fani hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: