Kituo cha faharasi na kupangilia maálumaat chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya semina kuhusu mitindo mipya ya faharasi kwa watumishi wa maktaba ya mkoa wa Basra, masomo yanahusu wasifu wa vitabu na usanifu pamoja na matumizi ya program ya (MARC 21 na RDA) nazo ni program za kisasa zinazo tumika katika maktaba sambamba na program ya (KOHA) inayo tumika kwenye maktaba kubwa za kimataifa.
Malengo ya semina hii –kwa mujibu wa wasimamizi- ni kuongeza elimu na kubadilishana uzowefu katika sekta hii, sambamba na kuwajulisha watumishi mbinu mpya zinazo tumika katika utaratibu wa faharasi, mbinu ambazo kituo cha faharasi na kupangilia maálumaat cha Atabatu Abbasiyya kinauzowefu nazo na kinaweza kuzifundisha kwa viwango vyote.
Semina hii imetokana na maombi ya uongozi wa maktaba ya mkoa wa Basra, pia ni sehemu ya mfululizo wa semina zinazo tolewa na kituo tajwa hapo juu kwenye maktaba za serikali na binafsi.