Wamepokelewa kwa mauwa na shangwe: Wageni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata mapokezi makubwa katika uwanja wa ndege wa Lahoor.

Maoni katika picha
Mwitikio wa wito wa kadhi mkuu wa Pakistani Dokta Sayyid Mudhwahhar Ali Akbaru Naqwiy, ugeni wa Atabatu Abbasiyya umewasili Pakistani, kuangalia hali za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), na kufungua daraja la undugu na mapenzi kati yao na watu wa Karbala, na kuwafikishia harufu nzuri ya malalo zake takatifu, huwenda wanaweza kuwapunguzia kiu kidogo waliyo nayo ya kumuona bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kuhusu ziara hii tumeongea na mjumbe wa ugeni huo Shekh Muhammad Jawaad Salaami ambaye ni mkuu wa kituo cha mahusiano ya kimataifa na mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika bara la Marekani kaskazini na kusini, amesema kua: “Ziara ya ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika nchi ya Pakistani inatokana na mwaliko rasmi kutoka kwa Kadhi mkuu wa Pakistani Dokta Sayyid Mudhwahhar Ali Akbaru Naqwiy, na sisi kama watumishi wa Ahlulnait (a.s) tunaona fahari kuja katika nchi hii kushirikiana na watu wake katika harakati zao za kiimani na kitablighi pamoja na kuwapa nafasi ya kutabaruku na athari za Maimamu waongofu (a.s) sambamba na kuangalia hali zao”.

Akaongeza kua: “Kupitia ziara hii tunategemea kufungua daraja la mawasiliano na taifa hili hasa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), tunatarajia kuwa na matokeo chanya katika ziara hii, tunaweza kusema ndio mwanzo wa kufungua ushirikiano baina yetu, pamoja na kufungua hali ya mawasiliano ya kiroho na watu ambao hawana uwezo wa kuja kutembelea Ataba tukufu katika mji wa Karbala”.

Mapokezi hayo yameripotiwa na vyombo vingi vya luninga na redio za Pakistani, wageni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu watakuwa na ziara ya siku mbili zaidi chini ya ratiba maalum iliyo jaa vitu vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: