Mwanafunzi kutoka Maahadi ya Quráni tawi la wasichana amekuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Quráni hapa Iraq.

Maoni katika picha
Mwanafunzi wa Quráni tukufu tawi la wasichana chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu Zaharaa Hussein, amekua mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuhifadhi Quráni tukufu (ya wasichana) wanafunzi wa sekondari (upili), yaliyo andaliwa na idara ya malezi ya mji wa Bagdad na mikoa mingine.

Mashindano yalikua na washiriki wengi kutoka idara zilizo chini ya wizara ya malezi, kulikua na mashindano mbalimbali ya mchujo (mtowano) hadi kupata washiriki wa mashindano ya mwisho yaliyo toa washindi wakuu, ushindi huo ni taji la kuongeza bidii katika usomaji wa Quráni tukufu na kuifanyia kazi.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa Maahadi ya Quráni tawi la wasichana wamesema kua: ushindi huu haujapatikana bure unatokana na juhudi kubwa zinazo fanywa pamoja na msaada endelevu wa kitengo hicho chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio weka ratiba maalum ya Maahadi katika tawi la wasichana na kuwaondolea vikwazo vyote sambamba na kuwawekea mazingira mazuri ya kuhifadhi Quráni, ushindi uliopatikana katika shindano hili ni kielelezo cha ratiba nzuri iliyo pangwa.

Kumbuka kua hii sio mara ya kwanza ambayo wasomaji wa Quráni wa Maahadi tawi la wasichana wanapata ushindi, kuna mashindano yaliyo fanyika siku za nyuma walipata ushindi pia, hii inaonyesha mfumo mzuri unaofatwa na Maahadi ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: