Watoto (313) wamehitimu masomo ya chekechea katika shule ya Saaqi na Durarul Ameed.

Maoni katika picha
Shule ya Saaqi na Durarul Ameed ambazo zipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu zinafanya hafla ya kuhitimu watoto (313) wakiume na wakike, imefanyika ndani ya ukumbi uliopo katika jengo la Shekh Kuleini (q.s) Jumanne asubuhi mwezi (24 Shabani 1440h) sawa na (30 April 2019m), na kuhudhuriwa na wahitimu pamoja na wazazi wao na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na viongozi wa malezi katika idara za Ameed.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, ukafuata ujumbe kutoka kitengo cha malezi na elimu ya juu, uliowasilishwa na Ustadh Wasim Abdulwahid Naafiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Leo tunashuhudia kuhitimu chekechea kwa kundi jipya la watoto wetu, tulilo liita (Kuzaliwa kwa miezi) kutokana na mazazi yanayo patikana katika mwezi wa Shabani, hakika masomo ya chekechea (awali) yana umuhimu mkubwa sana katika kumwandaa mtoto kwa ajili ya masomo ya msingi, kwani hupata maandalizi kamili yatakayo msaidia katika safari yote ya elimu”.

Akaongeza kua: “Hafla sio kwa ajili ya sherehe peke yake bali ni sehemu ya kuonyesha walicho jifunza, mambo mtakayo yaona hapa ni sehemu za masomo yaliyo fundishwa, hatuwezi kuongea mengi zaidi ya kutoa shukrani za dhati kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio tupa malezi ya mzazi kwa wanae, na tunakishuru kitengo cha malezi na elimu ya juu, pamoja na idara ya masomo ya chekechea (awali) kwa juhudi kubwa walizo fanya katika kuwafundisha watoto hawa, vilevile shukrani za dhati ziwaendee wazazi na walezi wa wanafunzi wetu walioshirikiana bega kwa bega na sisi katika kuwalea watoto hawa”.

Hafla ilikua na vipengele vingi vilivyo onyeshwa na wanafunzi, kulikua na kaswida, maigizo na video, mwisho kabisha wanafunzi wanao ingia darasa la kwanza walikabidhi bendera kwa wanafunzi wa chekechea wa shule zote mbili, shule ya Saaqi na Durarul Ameed.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: