Kuhitimisha mashindano ya kijana wa Alkafeel ya mwaka wa tatu.

Maoni katika picha
Kwa lengo la kukuza uwelewa wa kielimu, kitamaduni, kidini na kujenga ushindani, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano na vyuo kwa kushirikiana na idara ya malezi ya mkoa wa Muthanna inafunga mashindano ya kijana wa Alkafeel ya mwaka wa tatu, ambayo wanafunzi wa kiume na wakike kutoka shule za sekondari walishiriki hivi karibuni.

Hafla ya kufunga mashindano hayo imefanyika ndani ya ukumbi wa marehemu Ahmadi Abduljaasim katika mji wa Samawah, ujumbe unaowakilisha Atabatu Abbasiyya umeshiriki, pamoja na mkuu wa idara ya malezi ya mkoa wa Muthanna, na viongozi wa idara mbalimbali za malezi, bila kuwasahau wanafunzi na wazazi wao, baada ya kusomwa Qur’ani ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na kusikiliza wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa idara ya malezi ya mkoa bwana Sa’adi Khadhwiri Rishawi, akasema kua: “Pongezi kwetu kwa kufanyika mashindano ya kijana wa Alkafeel mwaka huu kwa wanafunzi wa mkoa wa Muthanna, tunashukuru na kupongeza kazi zinazo fanywa na Ataba kwa vijana wetu, pamoja na kuwepo kwa hisia za kiimani kwa kila kazi njema inayo fanywa, matarajio yetu ni kuona jambo hili linarudiwa tena siku za usoni kwa wanafunzi wetu”.

Halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Kamali Karbalai kutoka kitengo cha Dini, akasisitiza kua: “Hakika tunapita katika zama zenye changamoto nyingi na hakuna njia ispokua kupambana nazo kwa kuonyesha malezi mema, tujifunze katika madrasa ya Ahlulbait (a.s), ili tuwe mfano mwema kwa kila mtu”.

Hafla ikafungwa kwa kuwapa zawadi washindi, washiriki wa mashindano hayo walikua wanafunzi (2000) wakiume na wakike, kutoka katika shule za sekondari za mkoa wa Muthanna, walioshinda ni wanafunzi (50) chini ya vigezo vilivyo wekwa na wasimamizi wa mashindano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: