Wizara ya elimu ya juu: Mahafali za kielimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu zinaendana na mtazamo wa wizara kuifanya elimu kua msingi wa uzalishaji.

Maoni katika picha
Wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu kupitia mkuu wa idara ya ukaguzi wa elimu imesema kua: “Hakika mahafali za elimu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya, ikiwemo mahafali hii, zinakubaliana na mtazamo wa wizara wa kuifanya elimu kua msingi wa uzalishaji, elimu za sasa; mwanafunzi anatakiwa kujifunza namna ya kua mzalishaji”.

Yamesemwa hayo katika ujumbe wa wizara ulio wasilishwa na Dokta Nabili Hashim Aárajiy raisi wa idara ya ukaguzi wa elimu, katika hafla ya ufunguzi wa mashindano ya kijana wa Alkafeel ya mwaka wa tatu, yanayo husu kazi za ubunifu, udaktari na uhandisi kwa wanafunzi wa vyuo vya Iraq, yanayo ratibiwa na Atabatu Abbasiyya kupitia idara ya mahusiano na vyuo ndani ya mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo, iliyo fanyika alasiri ya leo (25 Shabani 1440h) sawa na (1 Mei 2019m) yatakayo fanyika siku mbili.

Akaongeza kua: “Nakipongeza chuo kikuu cha Al-Ameed kwa mtazamo huu ambao unaonyesha kuwajali vijana, na namna wanavyo saidia sekta ya elimu, kila mtu anajua umuhimu wa tafiti za kielimu katika vyuo, miongoni mwa vipaombele vya serikali ni tafiti za kielimu, sasa hivi kunavigezo vya kimataifa kuhusu ubora wa tafiti za kielimu, na kuna majarida ya kimataifa yaliyo pasishwa kutangaza tafiti za kielimu”.

Akafafanua kua: “Ni wazi kua, umuhimu wa tafiti za kielimu unaonekana kwa kiwango cha tafiti zinazo fanywa, maendeleo mengi duniani hutokana na tafiti za kielimu, hata maendeleo ya nchi yanategemea tafiti fizo kwa kiwango kikubwa, taifa hupimwa uwezo wake kwa kuangalia vitu wanavyo tengeneza kutokana na utafiti wao, utafiti wa kielimu umekua sawa na utambulisho wa taifa, chuo na mtafiti husika, utafiti unaotangazwa katika jarida la kimataifa unatosha kuonyesha kua mtafiti anauwezo mkubwa wa kielimu na anaweza kutekeleza jambo hilo kimataifa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: