Chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Chuo kikuu cha Karkuuk kinafanya nadwa kuhusu kuishi kwa usalama raia wa Iraq.

Maoni katika picha
Kutokana na kuadhimisha mwaka wa tatu tangu kukombolewa mji wa Bashiri kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, asubuhi ya Alkhamisi ya (26 Shabani 1440h) sawa na (2 Mei 2019m) kimefanya nadwa ya kusisitiza kuishi kwa amani na usalama raia wa Iraq, chini ya kauli mbiu isemayo: (Kuishi kwa usalama baina ya nadhariyya na utekelezaji), katika kitivo cha katiba kwenye chuo kikuu cha Karkuuk na kufadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, imehudhuriwa na watafiti kutoka ndani na nje ya mkoa huu pamoja na wakufunzi na wanafunzi cha chuo.

Baada ya kusoma Qur’ani ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na kusikiliza wimbo wa taifa, kulikua na ujumbe wa Atabatu Husseiniyya tukufu uliowasilishwa na Shekh Ali Kar’awi, alisisitiza ulazima wa kuishi kwa amani na usalama, kutoa ushahidi katika historia ya kiislamu kwa kuanza na hadithi ya Ali (a.s) isemayo: (Watu wapo makundi mawili imma ni ndugu yako katika Dini au ndugu yako katika uumbwaji), jambo hili lilionekana katika kuitikia fatwa ya kulinda maeneo matakatifu, watu walijitokeza kila sehemu kuja kukomboa mji wa Bashiri, kwa sababu ndugu zao walikua katika hatari, hakika walifuata mwenendo wa Karbala, ulikua utukufu kwao kutekeleza fatwa ya Marjaa Dini mkuu, ambayo ndio msingu wa kuirudisha Iraq na kupata amani na usalama.

Kisha wakaendelea kupanda jukwaa watafiti mbalimbali ambao waliongeo mada tofauti, lakini jambo kubwa wote wamehiza kuishi kwa amani na mshikamano, kikao cha nadwa kiliongozwa na Dokta Twala’at Jayadi Alhadidi mkuu wa kitivo cha katiba katika chuo kikuu cha Karkuuk, miongoni mwa walio ongea ni:

  • - Abu Imaad Faraju Bulisu Inadi, mada isemayo: (Kuishi kwa amani na kulipenda taifa ni kitu kimoja).
  • - Dokta Imaad Dhwalimi, mada isemayo: (Kuishi kwa amani ni somo la kisaikolojia).
  • - Dokta Dalshadi Jalali, mada isemayo: (Haki za binaadamu katika kuishi kwa amani).
  • - Dokta Muhammad Jawadi Zainul-Aabidina, mada isemayo: (Kuishi kwa amani nchini Iraq baada ya ugaidi).

Mwisho wa nadwa, mkuu wa chuo alitoa zawadi kwa Atabatu Abbasiyya pamoja na watoa mada za kitafiti na wasimamizi wa nadwa hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: