Darul Kafeel ya Tarjama iliyo anzishwa miaka mitatu iliyopita chini ya kituo cha utamaduni na habari za kimataifa Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, hadi sasa inamachapisho zaidi ya (100) katika lugha (10) na kuwafikia zaidi ya watu bilioni tatu wanao zungumza lugha hizo kama lugha mama.
Hii ni mara ya kwanza kwa Darul Kafeel ya Tarjama kushiriki katika maonyesho haya ikiwa ni miongoni mwa matawi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Jassaam Muhammad Saidi kiongozi wa matawi ya Ataba tukufu yanayo shiriki katika maonyesho haya amesema kua: “Hakika machapicho ya Darul Kafeel yamekua na mwitikio mzuri, ukizingatia kua huu ni ushiriki wao wa kwanza, pamoja kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho haya, imekua ikishiriki tangu mwaka 2005, watu kutoka nchi za kigeni wametembelea kwa wingi tawi la Darul Kafeel hasa raia wa China.