Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) amempongeza Hujjat Islaam Shekh Ahmadi Marwi kwa kupewa cheo cha uongozi mkuu (sadana) wa Atabatu Radhawiyya tukufu, na kumtakia mafanikio katika kazi yake, na kumtaka aendeleze mema yaliyo anzishwa na watangulizi wake katika malalo hiyo ya Imamu wa nane Ali Ridhwa (a.s).
Ameyasema hayo katika ugeni aliouongoza kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliojumuisha wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya, walio kwenda kumpongeza Hujjat Islaam Shekh Ahmadi Marwi kwa kupewa cheo cha usimamizi (sadana) wa malalo takatifu ya Imamu Ali Ridhwa (a.s).
Kikao hicho kilihusisha viongovi wa Ataba za Iraq na Ataba tukufu za Iran, wakabadilishana mawazo na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika kuwahudumia wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka kila sehemu ya dunia, wakaongelea pia umuhimu wa ziara zinazo fanywa Iraq na Iran. Pamoja na kuangalia wepesi wanao fanyiwa mazuwari wa Iran waendapo Iraq au kunyume chake, hasa katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu kama vile ziara ya Arubainiyya, kwa mujibu wa Shekh Marwi, ziara hiyo ni kielelezo kikubwa cha ukarimu na mapokezi mazuri waliyo nayo watu wa Iraq kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mwisho wa maongezi yao kila upande ulimuomba Mwenyezi Mungu aneemeshe nchi zetu za kiislamu na kudumisha amani na usalama pamoja na kuongeza zaidi maendeleo.