Katika mwendelezo wa program zinazo lenga kutatua changamato zinazo patikana katika familia za wairaq, na kusaidia kujenga familia bora kwa kupitia ndoa, kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinatangaza kuanza usajili wa wanaotaka kujiunga katika program ya (Tengeneza furaha kwa mikono yako) kwa wanafunzi na watumishi wa vyuo, kwa ajili ya kuwaandaa wanaotarajia kuingia kwenye ndoa na kuwafanya waweze kua wanandoa bora, watakao jiepusha na mizozo ya ndoa na kifamilia ambayo husababisha kuvunjika ndoa na kuharibika kwa familia, program itaanza baada ya likizo ya sikukuu ya Idil-Fitri Insha-Allah.
Program itakua na hatua mbili:
Hatua ya kwanza: (Misingi ya kujenga mtu salama).
Hatua ya pili: (Misingi ya maisha ya familia).
Katika program hiyo kutakua na maswali pamoja na mashindano, zawadi zitatolewa kwa washiriki.
Program itafanyika siku mbili kila wiki, usafiri wa kuwachukua na kuwarudisha washiriki majumbani kwao utakuwepo, na wanaotoka nje ya mkoa wa Karbala wataandaliwa malazi na chakula, pia watapata nafasi ya kufanya ziara na kutembezwa katika miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Jiandikishe kwa kutumia namba ya simu ifuatayo: 07828884555 (Viber, Whatsapp, Telegram).
Sehemu kilipo kituo: Karbala tukufu/ mtaa wa Mulhaqu/ barabara ya hospitali ya Hussein/ jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah/ ghorofa ya tano.