Nukta muhimu alizo ongea Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya swala ya Ijumaa.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) mwezi (27 Shabani 1440h) sawa na (3 Mei 2019m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ameongea vipengele vingi vya kimaadili na kimalezi vinavyo husu mazingira halisi tunayoishi, miongoni mwa aliyo ongea ni:

  • - Kitabu, mwalimu na familia ni vitu muhimu katika kujenga uwelewa wa mtu.
  • - Kitabu bado kinaendelea kua nguzo muhimu ya kujenga uwelewa.
  • - Mwalimu ni nguzo ya pili katika kujenga uwelewa wa mwanaadamu.
  • - Malezi ni nguzo ya tatu na muhimu katika kujenga mfumo wa uwelewa, mwanaadamu hujifunza kutoka kwa babu, baba, mama na watu wengine ndani ya familia yake.
  • - Mtu hujifunza kutoka kwa wazazi wake adabu za kula pia hujifunza na mambo mengine.
  • - Kitabu, mwalimu na familia ni nguzo za uwelewa za asili.
  • - Ulimwengu wa leo umeshuhudia nguzo ya uwelewa mpya haikuwepo zamani na imezirahisisha nguzo za uwelewa.
  • - Hakika mapinduzi ya elimu ya sasa kupitia Intanet na mitandao ya mawasiliano ya kijamii imekua nguzo mpya inayo unda mfumo wa uwelewa ambayo hauwezi kukanusha athari zake.
  • - Sehemu kubwa ya vyanzo vya habari katika mitandao hazina utambulisho, na inashawishi fikra pamoja na kupingana taarifa zake.
  • - Hakika uwelewa unaotokana na mitandao ya kijamii sio sawa na uwelewa unaotoka kwa mwalimu.
  • - Mitandao ya kijamii ni rahisi kuitumia na ina athari kubwa.
  • - Utamaduni wa mitandao ni hatari sana kwa sababu kuna hadari mchanganyiko zisizokua na vyanzo vya kuaminika.
  • - Kila kitu huwekwa kwenye mitandao na kuna watu huongea maneno machafu yasiyo faa kabisa.
  • - Kuna watu wanamiliki zaidi ya peji moja katika mtandao mmoja kwa ajili ya kuweka mambo yanayo kinzana na kuchafua watu.
  • - Utamaduni wa mitandao hauna adabu ya lugha hata kidogo.
  • - Mwalimu hurekebisha makosa ya mwanafunzi ya maneno, maandishi hadi fikra.
  • - Mitandao inachochea matumizi mabaya ya lugha na kuacha tamaduni za asili.
  • - Baadhi ya watu huogopa kuongea maneno machafu mbele ya watu lakini wanapokua kwenye mtandao wanaweza kuandika maneno machafu kwa sababu hawaonekani na hawajulikani.
  • - Jamii inaweza kupata matatizo mengi kama itatekwa na mitandao na kuiamini katika kila jambo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: