Kupandishwa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa (Jahanki-Shaaha) uliopo mashariki ya Salikuti Pakistani.

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliopo Pakistani umepandisha bendera ya kubba ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika anga la mji wa (Jahanki-Shaaha) uliopo mashariki ya Salikuti Pakistani, umbali wa kilometa (500) kutoka mji mkuu wa Pakistani Islamabad.

Pamoja na ubovu wa barabara na mvua zinazo endelea kunyesha na giza la usimu, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na Imani imara waliyo jifunza kutoka kwa bwana wao Abbasi (a.s) wamewasili katika ngome ya wapenzi na wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) katika miji ya mbali kabisa, ili kuingiza furaha katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa (Jahanki-Shaaha).

Wamepata mapokezi makubwa sana, watu walifurika kwa shauku kubwa huku wakibubujikwa machozi, na kunyoosha mikono ili watabaruku japo kwa kugusa bendera ya kubba Abulfadhil Abbasi (a.s), waliweka maua pembezoni mwa barabara ikiwa kama ishara ya kuonyesha mapenzi yao, walisimama njia nzima watoto kwa wazee wanawake kwa wanaume huku wakipiga vigeregere na kusema (Labbaika yaa Hussein.. Labbaika yaa Abbasi).

Ndio.. ugeni wa watumishi wa Abbasi (a.s) umepokewa kwa shangwe na vifijo, kisha wote wakaelekea msikitini kuswali Magharibaini kwa jamaa chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Muhammad Jawaad Salami (d.t), baada ya swala ikaanza shughuli ya kupandisha bendera ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika anga la mji huu, asilimia kubwa ya wakazi wa mji huo wanatokana na kizazi cha Imamu Hussein (a.s), Shekh Salami akatoa shukrani kwa niaba ya wageni kutokana na mapokezi mazuri waliyo pewa pamoja na kuwatambulisha wageni na sababu ya kuja kwao, akafafanua utukufu wa kushikamana na wilaya ya Ahlulbait (a.s) pamoja na mwenendo wa Hussein (a.s) ambaye ndiye safina ya uongofu katika umma huu, akawafikishia salam za mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, akawaahidi baada ya kurudi kwao watafanyiwa ziara kwa niaba katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Naye bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan rais wa kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya akaongea kwa ufupi kuhusu namna Ataba tukufu zinavyo tilia umuhimu wa kutuma ujumbe wa kibinaadamu na kudumisha mawasiliano na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kila sehemu ya dunia.

Kisha watu wote wakaelekea katika Husseiniyya ya Qasri Abu Twalib (r.a) kupandisha bendera ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya mahudhurio makubwa ya wakazi wa mji huo, wageni wakagawa zawadi nyingi za kutabaruku kutoka katika haram ya Alkafeel (a.s), halafu wageni wakaagwa kwa huzuni huku wengine wanalia na kuomba isiwe mara ya mwanzo na mwisho kwa ugeni huo kuja katika mji huu.

Fahamu kua lengo la ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu tuja hapa Pakistani ni kuwasiliana na wafusi wa Ahlulbait (a.s), wale ambao hawawezi kwenda Iraq kufanya ziara katika Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: