Miongoni mwa miradi inayo fanywa na kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu na wenye mwitikio mkubwa ni mradi wa (pamoja na vijana), unaoangalia matatizo na changamoto za kitamaduni, kidini na kiitikadi kwa vijana, pamoja na kuangalia namna ya kuzitatua na kuwafanya wawe macho daima, sambamba na kuwaongezea maarifa mbalimbali, miongoni kwa vipengele vya mradi huo ni kushirikiana na wanafunzi wa vyuo vikuu katika kufanya maradi mbalimbali.
Kama ilivyo fanyika katika chuo kikuu cha Kufa, ambacho kilikua mwenyeji wa mkutano wa kamati ya waandishi ya habari, na washiriki wa mkutano huo ni wanafunzi pamoja na wakufunzi wao.
Mkutano ulilenga kujenga uwezo wa wanafunzi wa uandishi wa habari kupitia mihadhara iliyotolewa na walimu waliobobea katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na aina za habari zinazo weza kuathiri jamii, na namna ya kupanga habari kwenye gazeti, pamona na namna ya kuandaa habari ya kwenye luninga (tv), sambamba na kuandaa vipindi vya kwenye luninga (tv) na redio, na kuangalia vipaji vya sauti, mambo yanayo saidia mustakbali wa wanafunzi kielimu, na kuwafungulia fursa mpya baada ya kuhitimu kwao.
Kumbuka kua mkutano huu umetokana na mawasiliano ya moja kwa moja na vijana na kuwapa fikra kuhusu mradi huu na mingine yenye lengo la kuinua uwezo wao katika nyanja tofauti.
Ufuatiliaji na uhariri: kamati ya wahariri wa mtandao wa kimataifa Alkafeel.