Raudhat Ahbaabul-Kafeel imefanya hafla ya wahitimu wake wa awamu ya sita.

Maoni katika picha
Kuandaa mwenendo wa maisha yenye mafanikio kwa watoto kielimu na kikazi, Raudhat Ahbaabul-Kafeel chini ya Maahadi ya Quráni tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya inafanya hafla ya wahitimu wake wa awamu ya sita, baada ya juhudi kubwa iliyofanywa na watumishi wa Raudhat hiyo, ya kufundisha watoto masomo na tabia nzuri kwa ajili ya kuwaandaa kujiunga na darasa la kwanza, huku wakiwa wamehifadhi juzu la thelatini la Quráni tukufu na kupambika na tabia nzuri.

Raudhat Ahbaabul-Kafeel ni moja ya Raudhat nyingi zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kutengeneza kizazi bora kinacho fuata maadili ya Quráni tukufu kuanzia mwanzo wa safari ya elimu ya watoto, wanazoweshwa kusoma Quráni tukufu tangu wakiwa bado wadogo, nayo ni moja kati ya shule za awali (chekechea) maalum hapa Iraq, inasimamiwa na watalamu walio bobea katika kuwaandaa watoto na kuwafundisha maadili ya Quráni pamoja na mambo mengine.

Hafla ilipambwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na kaswida na maigizo kutoka kwa watoto wakiwa na furaha kubwa wao na wazazi wao.

Ufutiliaji na uhariri: kamati ya wahariri ya mtandao wa kimataifa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: