Mashindano yataanza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na yataendelea mwezi mzima, kuna zawadi zimeandaliwa kwa ajili ya washindi baada ya kupiga kura, ambazo ni:
Mshindi wa kwanza na wa pili: Kwenda Umra katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kutembelea kaburi la Mtume (s.a.w.w).
Mshindi wa tatu: Kwenda kumtembelea (kumzuru) Imamu Ridhwa (a.s).
Mshindi wa nne: kwenda kumtembelea (kumzuru) bibi Zainabu (a.s).
Pamoja na kuzingatia yafuatayo:
- 1- Mshiriki anamaamuzi ya kusoma yeye mwenyewe (mubashara) moja kwa moja au kusikiliza na kufuatiliza kisomo katika vikao vya usomaji wa Quráni ndani ya Ataba tukufu na maeneo mengine, au kupitia visomo vya kwenye mtandao vinavyo fanywa na Maahadi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
- 2- Wakati wa kusoma khitima mbili unaweza kuweka nia tatu, ya kwako na wazazi wako wawili.
- 3- Kuchagua khitima moja tuma namba (1) na khitima mbili tuma namba (2).
- 4- Unapo maliza kusoma khitima tuma neno (tayali).
- 5- Niaba inasihi kwa waliohai na waliokufa.
- 6- Watafanyiwa ibada za umra na ziara ya kaburi la Mtume (s.a.w.w) kwaniaba watu wote watakao shiriki, pamoja na ziara ya Imamu Ridhwa na bibi Zainabu (a.s).
- 7- Washindi (wa kwanza, wa pili, wa tatu na wa nne) watapatikana kwa kupiga kura ya washiriki.
Kwa maelezo zaidi piga simu zifuatazo: (07731881800 / 07805776518).
Au wasiliana nasi kwa mitandao ifuatayo:
1- t.me/turathmanage
2- WhatsApp، Viber—07731881800
3- https://www.facebook.com/1115686655150464/posts/2386988851353565/
Ufuatiliaji na uhariri: kamati ya wahariri ya mtandao wa kimataifa Alkafeel.