Katika ujumbe wa Mheshimiwa katibu mkuu ameongea mambo mengi kuhusu watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ujumla amehimiza kuongeza juhudi na kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru, miongoni mwa aliyo sema ni:
- - Viongozi wa idara ndio kiunganishi kati ya mtumishi na Ataba, eneo hilo likiimarika huwa na matokea mazuri.
- - Mnatakiwa kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya kazi na ibada.
- - Mjiandae kuwahudumia mazuwaru wanaokuja mchana na usiku ndani ya mwezi huu mtukufu.
- - Nyie ndio picha ya Atabatu Abbasiyya tukufu mnatakiwa mjipambe na jukumu hilo.
- - Mpambike kwa maadili mema, fikra nzuri na utekelezaji bora wa mafundisho ya Dini.
- - Muongeze kuheshimiana baina yenu na mazuwaru na muhakikishe hali hiyo inadum.
- - Mlinde mali za Atabatu Abbasiyya tukufu zilizopo ndani ya haram au nje kwani mali hizo ni wakfu wa mwenye malalo.
- - Mlinde heshima ya eneo hili takatifu wala msijihusishe na mzozo au mlengo wowote.
- - Zaairu ni bwana na sisi watwana, namna gani mtwana anavyo mtumikia bwana wake.
- - Miradi ya Atabatu Abbasiyya inamafanikio makubwa na maadui wa mafanikio ni wengi, tunatakiwa kulinda mafanikio hayo.
Pia kulikua na maelekezo kutoka kwa wajumbe wa kamati kuu, miongoni mwa waliyo sema ni:
- - Yatupasa kushukuru kwa kupata nafasi ya kutoa huduma sehemu hii takatifu, namna ya kushukuru ni kufanya kazi kwa uaminifu (ikhlasi).
- - Tunatakiwa kunufaika na kila fursa ndani ya kipindi hiki kitukufu.
- - Kiongozi wa idara anajukumu la ubaba, anatakiwa aongoze vizuri idara yake.
- - Lazima tuimarishe usalama.
- - Kuongeza uwezo wa wafanyakazi kulingana na sekta zao.
Baada ya hapo ukafunguliwa mlango wa majadiliano na maswali, viongozi wakatoa ufafanuzi zaidi na kujibu maswali pamoja na kuahidi kufanyia kazi mambo yenye faida kwa wote.