Wageni kutoka taasisi ya Swadaqat Dauliyya watembelea hospitali ya rufaa Alkafeel.

Maoni katika picha
Ugeni kutoka taasisi ya Swadaqat Dauliyya pamoja na jopo la wajumbe na viongozi wa mkoa wa Karbala na Baabil wametembelea hospitali ya rufaa Alkafeel wakiwa pamoja na kiongozi wa habari Ustadh Khabbaaz.

Mkuu wa ofisi ya taasisi ya Swadaqat Duwaliyya tawi la Karbala Ustadhat Ikhlas Asadiy amesema:

Taasisi ya Dokta Ali Wasaaf imetuma wajumbe kutoka mkoa wa Baabil na Karbala walio fanya ziara na kiongozi wa habari Ustadh Ali Khabbaaz katika hospitali ya rufaa Alkafeel ili watume picha ya wazi kuhusu hoapitali hiyo baada ya kupata maelezo kamili kuhusu huduma inazo toa kwa wananchi watukufu, imekua wazi kwetu kua baadhi ya huduma zinagharama kubwa, kwa sababu ya baadhi ya madaktari kuomba hela kubwa ambazo hazihusiani na hospitali, kutokana na baadhi ya wagongwa kujichagulia dotka maalum, pia tumeona namna madaktari wanavyo wajali wagonjwa na kuwapa huduma bora zaidi.

Akaongeza kua: Tukatembelea kitengo maalum cha kupandikiza chembechembe hai, tunategemea wizara ya afya ishirikiane na hospitali ya Alkafeel ili kitengo hicho kianze kazi na kuokoa gharama za kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu hayo, pia imependekezwa kutumia bima za afya kwani zinaumihimu mbwa kwa wakazi wa Karbala na Iraq kwa ujumla.

Kumbuka kua makao makuu ya taasisi ya Swadaqat Duwaliyya ipo nchini Swiden.Sajjaad Twalib Halo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: