Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: ((Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Quráni kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)), hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amewawekea waja wake muda maalum wa kushindana katika kufanya mambo ya kheri, na kuongeza ibada, miongoni mwa nyakati hizo ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa Quráni, kheri, baraka, sadaka na dua, hakika ni mwezi wa visimamo, mwezi wa kufanyiana wema, mwezi wa kuachwa huru na moto kwa atakaye tubu na kurejea kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Enyi waumini: tunatakiwa tuishi vizuri katika mwezi huu mtukufu, mgeni huyu mkarimu huondoka haraka, siku mbili au tatu zilizo pita tulikua tunasema: kesho au baada ya kesho utaandama mwezi wa Ramadhani, na baada ya siku chache tutasema: umeisha mwezi wa Ramadhani, hakika huu ni mwezi wa kheri, mwezi wa baraka, rehma zake huja haraka na kuondoka haraka, Allah Allah katika siku hizi, Allah Allah katika mwezi wa Quráni, Allah Allah katika mwezi wa funga, Allah Allah katika mwezi wa kuswali… imepokewa katika khutuba ya Mtume (s.a.w.w) ya kupokea mwezi wa Ramadhani, kama ilivyo hadithiwa na Huru Aamiliy katika kitabu cha Wasaaili Shia (juz 10/uku 313) amesema (s.a.w.w): (Hakika umekujieni mwezi wa Mwenyezi Mungu na Baraka, rehma na maghfira, mwezi bora mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda miezi yoto, na usiku wake ni bora kushinda usiku zote, na mchana wake ni bora kushinda michana yote, na saa zake ni bora kushinda saa zote, ni mwezi ambao mmeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu, na amekujaalieni katika wakirimiwa wake, pumzi zenu katika mwezi huu mnaandikiwa thawabu za tasbihi, na usingizi wenu ni ibada, ibada zenu zinakubaliwa, na dua zenu zinajibiwa, muombeni Mwenyezi Mungu Mola wenu kwa nia za kweli, na nyoyo safi akuwezesheni kufunga na kusoma kitabu chake.
Hakika muovu zaidi ni yule ambaye hatapata msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu mtukufu, kutokana na njaa yenu na kiu chenu kumbukeni njaa na kiu ya siku ya kiyama, wapeni sadaka mafakiri na masikini wenu, waheshimuni wakubwa wenu na wahurumieni wadogo wenu, ungeni undugu wenu na hifadhini ndimi zenu, msiangalie visivyo kua halali kuangaliwa, wala msisikilize yasiyokua halali kusikilizwa, wahurumieni mayatima na watu watawahurumia mayatima wenu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu dhambi zenu na mnyanyue kwake mikono yenu kwa kumuomba).