Je unapenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kufanya ibada za mwezi mtukufu wa Ramadhani?

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa wito kwa wapenzi na wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) mashariki na magharibi ya ardhi, wale waishio mbali na hawawezi kuja katika ardhi ya kujitolea (Karbala) kufanya ziara kwa bwana wa vijana wa peponi na ndugu yake mwezi wa familia (a.s), wajiandikishe majina yao kwa ajili ya kufanyiwa ziara, pamoja na kusoma dua Iftitaah na ziara ya Imamu Ali (a.s) katika siku ya kifo chake, na ziara ya Imamu Hassan (a.s) katika kuadhimisha kuzaliwa kwake, pamoja na ziara maalum katika siku za Lailatul Qadri na usiku wa Idil-fitri na mchana wake.

Mtandao umeandaa watu watakao fanya ziara kwa niaba ya kila atakaye andikisha jina lake katika ukurasa wa ziara kwa niaba kupitia linki ifuatayo: (http://alkafeel.net/zyara).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: