Kwa picha: Kazi ya kuweka marumaru sehemu ya mwisho katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeanza.

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza kiwango kikubwa cha kazi za awali za sehemu ya tano na ya mwisho katika kazi za kuweka marumaru haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi ambayo imechukua muda mrefu kutokana na umuhimu wake pamoja na umakini katika utendwaji wake, hasa katika mambo yanayo husiana na utowaji wa huduma pamoja na kuondoa marumaru za zamani na kurekebisha sehemu zilizo haribika, na kuweka zege maalum linalo saidia kushikana vizuri na ardhi ya zamani na inayo zuwia unyevu nyevu, mafundi wameanza kazi ya kuweka marumaru katika eneo la kusini kati ya mlango wa Kibla na mlango wa Imamu Hassan (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Mhandisi Dhiyau Majidi Swaaigh amesema kua: “Hakika kazi inaendelea vizuri na tunatarajia kumaliza siku chache zijazo, tunafanya kazi kwa umakini bila kutoa usumbufu kwa mazuwaru watakao ongezeka katika mwezi huu wa Ramadhani”.

Akasisitiza kua: “Kazi inafanywa kama ilivyo pangwa, inahitaji umakini mkubwa katika utekelezaji wake, hasa katika sehemu za kuunganisha mifumo ya kutoa huduma”.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni miongoni mwa miradi inayo kamilisha miradi iliyo tangulia, umefanywa kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani kuliko pelekea kuharibika kwa muonekano wake kutokana na ukongwe wake, kwani zinazaidi ya miaka (50), ndipo uongozi wa Atabatu Abbasiyya ukaamua kufanya mradi huu, kwa ajili ya kupendezesha muonekano wake kwa kiasi ambacho itaburudisha nyoyo za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: