Minara ya malalo mawili takatifu Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) inakaribisha kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Ewe mwezi wa funga tubashirie kwa nuru za swaumu

Marhaba yaa marhaba inatamkwa na kila anaamu

Maukibu ya nuru inaongoza baina ya tahlili za ibaad

Mapenzi ya ukaribisho yanaambatana na ayaat widaad

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa beti hizo, mwezi wa rahma, maghfira na ibada, niutamaduni uliozoweleka kila unapo karibia mwezi mtukufu wa Ramadhani, watu waliopo katika malalo mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na wale waliopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, husoma mashairi, kaswida na dua za kuukaribisha mwezi mtukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na wengine hufuatilia kupitia luninga zao.

Pia hutolewa mafundisho maalu ya Dini kabla ya Dhuhuraini na Maghribaini kuhusu mwezi wa Ramadani mtukufu, huzungumzwa umuhimu wa funga na utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu, pamoja na kutoa uthibitisho kutoka ndani ya Quráni tukufu na katika hadithi za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: