- 1- Fikra ya filamu iendane na kauli mbiu ya kongamano.
- 2- Filamu ionyeshe ushujaa wa wanajeshi na hashdi Shaábi katika kulinda taifa, misingi ya ubinaadam, mazingira na maeneo matakatifu kwa ujumla bila kuelemea upande wowote.
- 3- Isiwe imeshawahi kuonyeshwa mitandaoni au kushiriki katika shindano lingine.
- 4- Iwekwe kwenye (CD) na kukabidhiwa kwenye kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasifu (cv) ya mtengenezaji wa filamu, au utumwe kwa barua pepe kwa anuani hii: alkafeelkids@gmail.com
- 5- Mwisho wa kupokea filam zitakazo shiriki ni (10 Juni 2019m).
- 6- Filamu isiwe chini ya dakika (3) na isizidi dakika (5).
- 7- Matukio ya ukatili na umwagaji wa damu yasionyeshwe wazi bali yawekewe pazia.
Kumbuka kua washindi watano wa kwanza watazawadiwa kiasi cha (400,000) dinari laki nne za Iraq kila mmoja.