Kufuatia kuingia mwezi wa fadhila: Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinafanya hamla ya Alwafaa kwa mashahidi.

Maoni katika picha
Viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinafanya hamla ya kiibada kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa jina la (Hamlatul wafaa lilshuhadaa), wametoa wito kwa waumini wa kumfanyia shahidi au mashahidi moja ya ibada zinazo suniwa kufanywa ndani ya mwezi huu mtukufu, kama vile: (swala, kusoma Quráni, ziara, dua, kutoa sadaka…).

Unaweza kufanya ibada na kuelekeza thawabu kwa mmoja wa mashahidi au kwa wote, hilo ni jambo dogo sana tunalo weza kuwafanyia watukufu hawa walio jitolea nafsi zao ili tuweze kufunga na kufanya ibada kwa amani na utulivu.

Unaweza kushiriki katika kufanya ibada hizo mubashara (moja kwa moja) au kwa kupitia mtandao wa (Whatsapp – Telegram) kwa namba hii (07801071822).

Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kufuatia kuingia kwa mwezi wa Ramadhani kimetangaza kugawa chakula kwa familia za mashahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: