Chuo kikuu cha Al-Ameed kinagawa chakula kwa familia masikini na za mashahidi katika mji wa Karbala.

Maoni katika picha
Kutokana na ratiba ya kuwajenga wanafunzi kiimani, kitengo cha mafundisho ya kinafsi na maelekezo ya kimaadili katika kitivo cha tiba/ chuo kikuu cha Al-Ameed kimeweka ratiba ya kugawa chakula cha mwezi wa Ramadhani, ambayo hutekelezwa na wanafunzi kuanzia mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kila mwaka.

Huondoka kundi la wanafunzi pamoja na mlezi wao wa kimaadili kwenda katika nyumba za mafakiri na familia za mashahidi ndani ya mji wa Karbala kutambua mahitaji yao na kuwapa misaada ya kiroho na kimali.

Kiongozi wa kitengo cha mafundisho ya kinafsi na maelekezo ya kimaadili katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Hassanaini Mussawi amesema kua: “Ratiba hii inahusisha kugawa vikapu vilivyo jaa aina mbalimbali za vyakula ambavyo tunatarajia vitawasaidia katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani”.

Akasema: “Hakika ziara hizi tunaamini kua zinawajenga wanafunzi kiroho na kimaadili, na kuwafanya wahisi kuwajibika kwa tabaka hili la watu katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: