Maoni katika picha
Mhadhiri wa kozi hii ni Shekh Mahmudu Dauriyab Najafiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Lengo la kozi hii ni kumjulisha mtafiti wa hauza au sekula misingi ya rijaliyya, kiasi cha kumpa uwelewa wa mambo haya ambayo ni muhimu sana katika sekta ya hauza”.
Akaongeza kua: “Tumewaalika wale wanao somea uhakiki na wanao penda kujua mambo haya, na sisi tunawasomesha kwa njia rahisi ili tusiwape uzito”.
Akamaliza kwa kusema kua: “Shukrani nyingi ziende kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kwa kuwa walezi wa kozi hii ya kielimu, na kutupatia kila kitu cha lazima katika kufanikisha masomo haya”.