Mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje ni sehemu kuu ya kufturu mazuwaru.

Maoni katika picha
Siku za Ijumaa na Lailatul-Qadri hushuhudia ongezeko kubwa la mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), barabara ya (Najafu – Karbala) ni lango kuu la kuingia katika mji huu mtukufu, kwenye barabara hiyo kuna vituo vya mkarim wa bani Hashim mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje, vituo hivyo hutoa huduma muhimu kwa mazuwaru wa Arubaini, na hivi sasa vinatoa huduma kwa mazuwaru waliofunga, vinagawa futari kwa mazuwaru hao.

Mkuu wa mgahawa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Jawadi Hasanawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Huduma hii ni miongoni mwa sehemu ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunaandaa futari mapema na kuigawa kwa mazuwaru katika usiku wa Ijumaa na Lailatul-Qadri, vilevile tumeandaa sehemu ya kufturu ndani ya ukumbi wa mbele ya mgahawa”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum katika mwezi mtukufu wa Ramadhani yenye vipengele vingi kikiwemo hiki cha kugawa futari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: