Wamefurika katika pepo ya ardhini na kupaza sauti zao kwa kuomba dua: Mazuwaru katika usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwenye Ataba tukufu za Karbala.

Maoni katika picha
Usiku wa Ijumaa hushududia ongezeko kubwa la mazuwaru wanaokuja katika malalo tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), hali itakuwaje usiku huo unaposadifu usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mazuwaru huongezeka maradufu tofauti na Ijumaa za zingine, walianza kumiminika baada ya swala ya Dhuhurain wakaendelea kufurika hadi karibu na muda wa Maghribain.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya kazi kubwa chini ya utaratibu uliowekwa na Atabatu Abbasiyya katika mwezi huu mtukufu, wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru na kuhakikisha wanatekeleza ibada za mwezi wa Ramadhani kwa amani na utulivu, hivyo wanahakikisha kuwepo kwa mazingira mazuri ya kiroho yanayo wawezesha kufanya ibada kwa unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: