Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa ya kujilinda yatoa wito wa kushiriki katika maonyesho.

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa wito kwa watalam wa kazi za mikono kuja kushiriki katika maonyesho ya kazi za mikono (kuchora na kutengeneza vitu), yatakayo fanywa katika kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda awamu ya nne, katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu kuanzia (26 – 27 Juni 2019m).

Kamati imeweka sifa na masharti ya kushiriki kama ifuatavyo:

  • - Ubao uchorwe kwa rangi ya mafuta au wa maji na uwe na ukubwa wa (sm 70x50) au (sm 100x120).
  • - Picha ionyesho tukio lililo fanywa na Hashdi Shaábi katika vita ya ukombozi dhidi ya magaidi wa Daesh.
  • - Tukio liwe linalo onyesha uzalendo.
  • - Watoto wanaruhusiwa kushiriki katika maonyesho haya madam picha zao zinaonyesha matukio ya Hashdi Shaábi yenye uzalendo.
  • - Picha zitumwe kwa njia ya telegram kwenye namba hii (07721127581) kwa ajili ya kuiwasilisha kwenye kamati ya maonyesho na kuikagua kama imetimiza masharti.
  • - Mwisho wa kupokea kazi ni siku tano kabwa ya kuanza kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: