Kitengo cha Dini kinatoa huduma za mafundisho mbalimbali katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimepanga ratiba maalu ya mwezi wa Ramadhani, inayo endana na utukufu wa mwezi huu, ratiba hiyo inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Kuweka vituo vya kujibu maswali ndani na nje ya haram tukufu.
  • - Kutuma watumishi wa kitengo kwenda kutoa mihadhara na kusoma dua kwenye husseiniya mbalimbali ndani na nje ya mji wa Karbala.
  • - Kuongoza swala za jamaa katika maeneo yaliyo andaliwa kwa ajili hiyo.
  • - Kutoa mihadhara (mawaidha) kwa mazuwaru kila siku ndani ya haram tukufu.
  • - Kutoa mihadhara kila siku kwa watumishi wa malalo.
  • - Kuweka watumishi wa kitengo upande wa wakina mama kwa ajili ya kurekebisha hijabu za mazuwaru na kuwakumbusha umuhimu wa hijaba na kulinda heshima ya eneo hili.
  • - Kutoa mihadhara katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kuhusu mafundisho ya Dini.
  • - Kuweka mafundisho mbalimbali ya Dini yanayo husu mwezi wa Ramadhani kwenye vioo (Screen) zilizopo ndani na nje ya Ataba tukufu.

Kumbuka kua lengo la ratiba hii ni kunufaika na utukufu wa mwezi huu, na kuhakikisha watu wanafanya matendo mema, kwa mujibu wa mafundisho ya Dini kutoka kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), na kunufaika na msimu wa ibada na dua ili kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: