(Msafara wa Alwafaa) katika mji wa Bagdad umekusanya familia za mashahidi katika futari, kutokana na kutambua kujitolea kwao na kuonyesha shukrani kwa familia hizo pamoja na kuwakumbuka mashahidi wao, umeandaa kikao na kugawa nguo kwa watoto wa mashahidi, sambamba na kufuturu kwa pamoja.
Familia zilizo shiriki katika kikao hicho zinakaribia (50) zikiwa na watoto zaidi ya (100) wajinsia zote, wate walipewa nguo walizo penda na kuzichagua wenyewe.
Kikao kilikua na mawaidha pamoja na kuelezea umuhimu wa mashahidi katika uhai wa umma, ofisi ya (Msafara wa Alwafaa) ya Bagdad imeahidi kufanya ratiba hii ya kibinaadamu na kiibada mara mbili kila wiki ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadani.
Fahamu kua (Msafara wa Alwafaa) unamatawi katika mikoa tofauti hapa nchini, ulianzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kutekelezwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kama sehemu ya kuzienzi familia za mashahidi na majeruhi kutokana na namna walivyo vitolea kwa ajili ya taifa, na kuwasaidia kwa hali na mali kadri tutakavyo jaliwa.