Toleo la ishirini na tisa la jarida la (Al-Ameed).

Maoni katika picha
Jarida la Al-Ameed linalo tolewa na kituo cha Al-Ameed Duwaliyyu Lilbuhuthi wa Dirasaat chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni limetoka (toleo la nane kwa mara ya ishirini na tisa) likiwa limejaa tafiti mbalimbali, pamoja na mlango maalum uitwao: (Mtume mtukufu –s.a.w.w- ni kigezo chema na dalili kuu).

Jarida hili linamada saba –zipo za lugha ya kiarabu na moja kwa lugha ya kiengereza- zimeeleza historia ya Mtume kwa kutumia maneno ya kitaalamu na kimashairi, pamoja na shuhuda mbalimbali za wakati wa uhai wake kwa kueleza matukio yaliyo badilisha jamii ya waarabu, kutoka katika jamii isiyokua na maendeleo, jamii iliyojaa ugonvi, ujinga, na kua jamii mpya inayo fanya uadilifu na usawa, jamii yenye elimu na maarifa, ikawa jamii inayo heshimu haki za binaadamu na kufuata sheria.

Fahamu kua jarida la Al-Ameed huandika tafiti mbalimbali, linatolewa na kituo cha Al-Ameed Duwaliyyu chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na limepasishwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: