Kufuatia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na utaratibu walio jiwekea Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Dini imegawa mamia ya vikapu vwa chakula kwa familia za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, chini ya ratiba ya kusaidia familia za mashahidi waliojitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matakatifu, sambamba na kugawa chakula hicho kwa familia za mafakiri na masikini.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Karbalai, akaongeza kusema kua: “Shughuli hii ni sehemu katika ratiba ya Atabatu Abbasiyya ndani ya mwezi wa Ramadhani, ugawaji wa chakula pia ni sehemu ya ratiba ndefu inayo husisha kuratibu misafara ya kwenda kutembelea familia za mashahidi na majeruhi kwenye miji yote hapa Iraq, kwa ajili ya kudumisha mawasiliano nao na kusaidia mahitaji yao kama sehemu ya kuonyesha kujali kujitolea kwao, ratiba hii ni mwitikio wa wito wa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye taka kupunguza shida za familia hizi”.
Akabainisha kua: “Kikabu cha chakula kinakua na aina tofauti za vyakula anavyo hitaji mtu aliye funga, kama nafaka za aina mbalimbali, mafuta na nyama, familia hizo zimetuma salamu na shukrani zao kwa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasimamizi wa shughuli hiyo, wameonyesha kufurahishwa sana na msaada huu”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba kamili ya kusaidia familia za mashahidi tangu ilipo tolewa fatwa ya jihadi kifaya hadi leo, imesha saidia maelfu ya familia ikiwa ni kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu na kusaidia mapambano dhidi ya magenge ya kigaidi.