Kituo cha utamaduni wa familia chafanya mashindano ya wanawake katika mwezi wa Ramadhani.

Maoni katika picha
Kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza mashindano ya wanawake chini ya kauli mbiu ya hadithi tukufu isemayo (Kila kitu kina msimu na msimu wa Qur’ani ni mwezi wa Ramadhani), ukizingatia kua Qur’ani tukufu ndio katiba na mwangozo kamili wa mwislamu, na familia ndio msingi wa jamii, kuna hadithi nyingi zinazo sisitizo kujenga familia imara yenye mshikamano, mashindano haya yataendelea hadi mwisho wa mwezi wa Ramadhani.

Kituo kimeweka vigezo utaratibu wa kushiriki katika mashindano hayo:

Maudhui zifuatazo kila moja itolewe ushahidi wa aya:

  • 1- Maisha ya ndoa yenye utulivu.
  • 2- Kuthibiti haki ya mahari kwa mwanamke.
  • 3- Njia za kutengana wanafamilia.
  • 4- Haki ya kunyonya kwa mtoto.
  • 5- Haki ya kucheza kwa mtoto.
  • 6- Athari ya wivu kwa watoto.
  • 7- Fani ya kuomgea na kuwapa mawaidha watoto.
  • 8- Kulea wazazi wawili na kuwatendea wema pamoja na kujiepusha kuwafanyia maovu.
  • 9- Faida za kuzuwia hasira.
  • 10- Kujiepusha na kuvunja undugu.

Kituo kimesema kua kinapokea majibu kupitia namba ya simu ifuatayo 07828884555 kwa njia ya (whatsapp, viber na telegram) majibu sahihi yatapigiwa kura kutafuwa washindi baada ya Idil-Fitri, kuna zawadi zimeandaliwa kwa washindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: