Siku ya kimataifa ya uuguzi: Chuo kikuu cha Al-Ameed kimesisitiza kua kitatoa kizazi cha wauguzi wenye uwezo ukubwa wa kutoa huduma za uuguzi.

Maoni katika picha
Kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Ameed kimesherehekea siku ya kimataifa ya uuguzi, kwa kufanya hafla kubwa ndani ya ukumbi wa chuo, iliyo hudhuriwa na rais wa chuo Dokta Jaasim Marzuki, pamoja na washiriki kutoka katika vyuo vya uuguzi vya serikali na binafsi ndani ya mkoa wa Karbala na kundi kubwa la wanafunzi na wakufunzi wao.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo fuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya wa (Lahnul-Iba), kisha ukafuata ujumbe wa rais wa chuo Dokta Jaasim Marzuki ambaye amewapongeza watumishi wa sekta hii ya kibinaadamu, akawaomba waendelee kutoa huduma hiyo, ukafuata ujumbe wa mkuu wa kitivo Dokta Naaji Yaasir Almiyahi, akaelezea umuhimu wa kazi ya uuguzi katika sekta ya afya, pamoja na umuhimu wa kuwasaidia wauguzi na kuwajali, chuo kinatoa wahitimu mahiri wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma ya uuguzi katika taasisi za afya na kwenye jamii.

Katika hafla hiyo kulikua na kipengele cha mashairi yaliyo somwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo cha uuguzi kutoka chuo kikuu cha Baabil, yaliyo husu kazi ya uuguzi na wauguzi, ikafuata filamu fupi kuhusu uuguzi iliyo andaliwa na chuo kikuu cha Al-Ameed kitengo cha habari na mahusiano, kisha yakafanyika maigizo mafupi ya kikundi cha Kafu kuhusu kazi ya uuguzi.

Hafla ikafungwa kwa kugawa vidali kwa mkuu wa kitivo cha uuguzi na rais wa chuo pamoja na wakuu wa vitivo vya udaktari na udaktari wa meno, na wakuu wa vitivo vya uuguzi kutoka vyuo vingine walio hudhuria hafla hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: