Usomaji wa Quráni katika Maqaam ya Hujjatu-Llahi katika ardhi.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha usomaji wa Quráni katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), ikiwa ni moja ya vituo vya usomaji wa Quráni vinavyo simamiwa na Maahadi ndani na nje ya mkoa wa Karbala, katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi amesema kua: “Kama mnavyo jua Atabatu Abbasiyya tukufu inathamini sana kueneza utamaduni wa Quráni, miongoni mwa juhudi zake ni kuweka vikao vya usomaji wa Quráni kila mwaka ndani ya mwezi wa Ramadhani, jambo hili linaongezeka mwaka baada ya mwaka kwa kuongeza idadi ya vituo vya kusama Quráni na aina za usomaji, sambamba na kuweka matangazo maalum katika baadhi ya chanel za luninga”.

Akaongeza kua: “Kisomo hiki kinaendeshwa kwa kushirikiana na kitengo cha Dini pamoja na kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ndani ya mwezi wote wa Ramadhani, linashiriki jopo la wasomaji mahiri walio fanya vizuri katika mashindano ya Quráni yaliyo simamiwa na Maahadi, pia kuna wageni mbalimbali wa kiume na wakike wanao hudhuria usomaji huo, hukusanyika kwa ajili ya usomaji wa Quráni kila siku baada ya swala za Dhuhurain”.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu imeweka ratiba maalum ya usomaji wa Quráni katika mwezi wa Ramadhani yenye vipengele vingi, kikiwemo kipengele hiki cha vikao vya usomaji wa Quráni tukufu, na kubaini vipaji vya usomaji pamoja na kuweka utaratibu wa kutunza vipaji hivyo, sambamba na kunufaika na mazingira ya kiroho yaliyopo katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: