Idara imebainisha kua, ugawaji ulikua kama ifuatavyo:
- 1- Msafara wa kuitikia wito wa Marjaiyya, ulio elekea katika mji wa Sabú-Buur chini ya kauli mbiu isemayo: (tulikuwepo tumebaki na ahadi tunatekeleza) ambako waligawa vikapu vya chakula (330) na nguo karibu (850) kwa mayatima wa Hashdi Shaábi na familia za masikini.
- 2- Msafara wa watoto wa Marjaiyya wakazi wa mtaa wa Kafaah, waligawa vikapu vya chakula (350) kwa familia za mashahidi na masikini katika vitongoji mbalimbali vya mji wa Bagdad, kwa kufuata orodha maalum iliyokua imesha andaliwa ya watu wenye mahitaji katika mtaa wa Nasri na Sab’u-Qusuur.
Huo ndio ufafanuzi wa misaada iliyo tolewa na idara ya ustawi wa jamii ofisi ya misaada katika mji wa Bagdad ndani ya wiki ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadani.