Miongoni mwa harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani: Mashindano ya turathi ya vikundi

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zinazo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani, ni kuratibu mashindano ya turathi ya vikundi chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, yanafanywa mwezi mzima wa Ramadhani katika uwanja wa nyumba za Abbasi -mujammaá Abbasi- (a.s), kwa ushiriki wa vikundi (24) kwa ajili ya kuzitambua turathi za Kiislamu na kuangazia baadhi ya sekta muhimu.

Mashindano yanafanywa kwa vikundi, kuna vikundi (24) vinavyo shiriki, kila kikundi kina watu watano, na kila kikundi kimepewa jina au laqabu miongoni mwa majina na laqabu za Abulfadhil Abbasi (a.s), kila kikundi kinaulizwa maswali kumi katika kila mzunguko, kundi linalo faulu linaendelea mzunguko unaofuata na linalo feli linatoka, wataendelea hivyo hadi fainali chini ya kamati ya majaji wenye uzowefu wa kusimamia mashindano ya aina hii.

Kuhusu muundo wa maswali, kamati imesema kua: “Maswali yapo ya aina tofauti, kama vile: (Viongozi na wanachuoni, shule za kidini, hukumu na mifano, nani msemaji?, vitabu na maktaba, idara na vitengo, ushairi na washairi, malalo na maqaam, wasomi wa Quráni na maarifa ya Quráni, maswali kwa ujumla) kuna kamati maalumu ya kuuliza maswali.

Zawadi ya kikundi kitakacho shinda ni kwenda kumzuri Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) na zawadi zingine, hivyo hivyo kwa washindi wa pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: