Kila siku katika mwezi huu wa fadhila: Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu anafundisha mada za kimaadili na kimalezi kutoka katika dua ya Abu Hamza Shimali.

Maoni katika picha
Tangu siku za kwanza za mwezi mtukufu wa Ramadhani, na mwendelezo wa jambo aliloanza mwaka jana, umeandaliwa mfululizo wa mihadhara inayo tolewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), mbele ya kundi la watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), husherehesha makusudio ya kimaadili na kimalezi kutoka kwenye dua ya Abu Hamza Shimali, sambamba na kuowanisha na visa vya ndani ya Quráni tukufu.

Mihadhara inatolewa kila siku katika ukumbi wa sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mihadhara hiyo inajenga uwelewa mkubwa wa dua hii, nayo ni miongoni mwa dua zilizo pokewa kutoka kwa Imamu Zainul-Aabidina (a.s), ni dua ya kutubu na kurejea kwa Mwenyezi Mungu na ina nafasi kubwa ya kurekebisha nafsi, inamaneno yanayo weza kubadilisha mwenendo wa mtu na kumfanya awe na adabu mbele ya Mwenyezi Mungu, na aweze kukiri madhambi yake.

Kumbuka dua hii –Abu Hamza Shimali- ni muhimu sana kwa waumini, nayo ni miongoni mwa dua ndefu zilizo pokewa kutoka kwa Imamu Sajjaad (a.s), kwa kunakiliwa na Abu Hamza Shimali, imependekezwa kusomwa nyakati za usiku katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, imethibiti kuwa Abu Swafiyya Dinari Alkufiy ndiye anaejulikana kama Abu Hamza Shimali, jina la Shimali linatokana na kabila lake ambalo ni tawi la kabila la Al-Azdi, alikua miongoni mwa wapokezi wa hadithi za Imamu Zainul-Aabidina, Imamu Baaqir, Imamu Swadiq na Imamu Kaadhim (a.s), alikua mwanachuoni mkubwa wa madhehebu ya Imamiyya na uislamu kwa ujumla, alikua kinara wa hadithi, fiqhi, fani za lugha na masomo mengine katika zama zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: