Katika mazingira mazuri ya kiroho ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na katika ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vinaendelea visomo vya Quráni kwa siku ya nane mfululizo, zinasikika sauti murua za usomai wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu ametuambia kuhusu usomaji huo kua: Usomaji wa Quráni unafanywa kutekeleza kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Atakaesoma aya moja ya Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani ataandikiwa thawabu sawa na aliyesoma Quráni nzima katika miezi ya kawaida), na kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na Maahadi ya vikao vya usomaji wa Quráni katika mwezi wa Ramadhani, Maahadi inatilia umuhimu mkubwa kisomo hiki kinacho fanywa kila siku saa kumi na moja jioni kwa kusoma juzu moja, imeandaliwa sehemu maalum ndani ya ukumbi wa haram tukufu ambayo imewekwa misahafu kwa ajili ya kuwawezesha washiriki kufuatilia usomaji, pamoja na kuandaa kipaza sauti na jukwaa linalo endana na usomaji wa Quráni tukufu.
Kamera ya Alkafeel imefika eneo hilo na inakuletea baadhi ya picha.