Maahadi ya turathi za Mitume na chuo cha Ummul Banina zinafanya nadwa ya kujadili changamoto za usomaji kwa njia ya mitandao.

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) na chuo cha Ummul Banina (a.s) cha wasichana, wanafanya nadwa ya wanafunzi wa Maahadi na chuo, kwa ajili ya kujadili changamoto za kusoma kwa njia ya mitandao na kuangalia namana ya kuzitatua.

Kiongozi wa Maahadi ya turathi za Mitume Shekh Hussein Turabi amesema kua: “katika nadwa hii tumepokea maswali kutoka kwa wanafunzi, ambayo yamejibiwa na kubainisha urahisi utakao kuwepo wakati wa kuamiliana na wanafunzi”

Akafafanua kua: “Nadwa iliyo fanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya inahusisha wanafunzi kutoka mikoa mitatu: Bagdad, Karbala na Najafu, tumeanza na mkoa wa Karbala na tumekutana na wanafunzi (100)”, akasema kua: “Kuna nadwa zitafanyika katika mikoa mingine pia”.

Nadwa ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa kaswida ya katuni ya mtoto Muhammad Mushtaaq kuhusu mapenzi ya kweli kwa majemedali wa Hashdi Sha’abi.

Halafu ukatolewa ujumbe wa kihauza na Shekh Hussein Asadi ambaye alihimiza elimu, na akatoa wito wa kusoma kila kinacho wezekana kwa bidii.

Baada yake ukawasilishwa ujumbe wa idara na Shekh Hussein Turabi, akatumia baadhi ya aya na riwaya zinazo bainisha wajibu wa elimu, ikiwemo khutuba ya kiongozi wa waumini kutoka katika kitabu cha Nahaju Balagha, akasisitiza umuhimu wa kufuata utaratibu wa kutafuta elimu kwa mwanafunzi na athari yake katika nafsi na familia, pamoja na tablighi za kwenye mitandao na zile za moja kwa moja, jukumu letu ni kunufaika na elimu za kisasa.

Nadwa ikahitimishwa kwa ujumbe uliowasilishwa na kiongozi wa idara ya watalamu wa mitandao pamoja na kutoa ufafanuzi wa namna wanavyo endesha mitandao.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: