Kuendelea kufanyika mashindano makubwa ya Qur’ani hapa Iraq.

Maoni katika picha
Kuendelea kufanyika mashindano ya Qur’ani ya vikundi awamu ya tano, yanayo simamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, yanafanyika kila siku kwenye ukumbi wa Abbasi, yanamahudhurio makubwa na ushindani mkali.

Mashindano haya ndio makubwa zaidi hapa nchini, kuna vikundi (16) vinavyo shiriki kutoka zaidi ya mikoa ishirini, mashindano bado yako mzunguko wa kwanza, watakao faulu wataingia mzunguko wa pili.

Yanarushwa katika luninga mbalimbali, yanapewa umuhimu mkubwa na wadau wote wa Qur’ani hapa Iraq.

Fahamu kua Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya hufanya harakati mbalimbali kuhusu Qur’ani katika kipindi chote cha mwaka mzima, hufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani, hutoa mihadhara na huendesha mashindano katika miji tofauti hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: