Kifo cha mama wa waumini bibi Khadija bint Khuwailid (a.s) kilitokea mwezi wa Ramadhani…

Maoni katika picha
Mwezi mtukufu wa Ramadhani una matukio kadhaa ya kihistoria, ya kufurahisha na ya kuhuzunisha na kuumiza, miongoni mwa matukio yaliyo umiza roho ya Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) ni kifo cha mama wa waumini mkewe kipenzi bibi Khadija (a.s), aliye fariki mwezi kumi Ramadhani, baada ya miaka kumi tangu kupata utume na miaka mitatu kabla ya kuhama (hijra), mama huyu mtakasifu aliondoka katika dunia na kuacha jeraha na huzuni kubwa kwa Mtume (s.a.w.w) na umma wa kiislamu kwa ujumla, alikua nguzo madhubuti kwake, kilicho ongeza huzuni zaidi kwa Mtume (s.a.w.w) kifo cha mama huyu kilitokea mwaka alio fariki Ammi yake Abu Twalib (r.a), aliye kuwa nguzo muhimu kwake kisiasa na kijamii.. Shekh Majlisiy mwandishi wa kitabu cha Biharul Anwaar ameandika kua, bibi Khadija alikua na nyumba inayo weza kuingia watu wote wa Maka wa kipindi kile.

Bibi Khadija ndio mtu wa kwanza kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu, imepokewa kutoka kwa Ibun Abbasi kua: {Mtu wa kwanza kumwamini Mtume (s.a.w.w) katika wanaume ni Ali (a.s) na katika wanawake ni Khadija (r.a)}, alivumilia mitihanihani ya utume pamoja nae, alishirikiana nae katika kazi yake na machungu yake, alivumilia maisha magumu yaliyo tokana na vikwazo vya Makuraishi kwao, na alijitolea mali zake zote kwa ajili ya uislamu, hakika yeye ni mfano bora kabisa kwa wanawake wa kiislamu, hakika bibi Khadija baada ya kuolewa na Mtume (s.a.w.w), alikua nguzo muhimu kwa Mtume katika kupambana na changamoto za Utume, alimpunguzia unyonge na kumsaidia kupambana na vikwazo alivyo kua anawekewa na makafiri wa kikuraishi.

Aliolewa na Mtume (s.a.w.w) mwezi kumi mfungo sita (Rabiul Awwal), akiwa na umri wa miaka arubaini, na Mtume (s.a.w.w) akiwa na miaka ishirini na tano, Mtume hakuowa mke mwingine katika kipindi chote cha uhai wa bibi Khadija (r.a) hadi alipo fariki, kuna ikhtilafu kuhusu idadi ya watoto aliozaa na Mtume (s.a.w.w), lakini ni wazi kua Kassim na Fatuma Zaharaa (a.s) ni miongoni mwa watoto aliozaa na Mtume (s.a.w.w), Kassim alikufa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w), na Mtume huitwa kwa jina lake (baba Kassim).

Bibi Khadija (r.a) anahadhi kubwa, Mtume (s.a.w.w.) amesema: (Wanawake bora duniani ni wanne: Maryam binti Imraan, Asiya mwanamke wa Firaun, Khadija binti Khuwailid na Fatuma binti Muhammad).

Baada ya kufa bibi Khadija Mtume (s.a.w.w) alimuandaa na kumuosha, alipotaka mumvisha sanda akaja malaika Jibrilu (a.s) akasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.. hakika Mwenyezi Mungu amekutumia salam na anakuambia: Ewe Muhammad sanda ya Khadija itatoka kwetu, hakika huyo alitoa mali zake katika njia yetu). Jibrilu akaja na sanda, akasema: (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hii hapa sanda ya Khadija, nayo imetoka peponi kazawadiwa na Mwenyezi Mungu).

Mtume (s.a.w.w) akamvisha shuka yake tukufu kwanza, kisha akamvisha sanda iliyo letwa na Jibrilu (a.s), akavishwa sanda mbili: sanda iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu na sanda ya Mtume (s.a.w.w), alifariki akiwa na umri wa miaka (65), akazikwa katika makaburi ya Hajuun katika mji wa Maka, Mtume (s.a.w.w) alishuka ndani ya kaburi lake na kumzika, wakati huo sunna ya kuswalia jeneza ilikua bado haijaanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: