Kituo cha utamaduni wa familia kimejitolea kusaidia watoto wasiokua na malezi ya kifamilia na kuwarudisha katika familia zao.

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimejitolea kutafuta dawa ya kinafsi na kimwili kwa watoto waliokosa malezi ya kifamilia na kulelewa na kikundi cha (Ruhamaau Bainahum), kisha kusaidia kuwarudisha katika familia zao na katika jamii kwa ujumla, baada ya juhudi kubwa zilizo fanywa na kikundi hicho kuwaandaa hadi wakafika hatua hiyo.

Mkuu wa kituo Ustadhat Ismahani Ibrahim ametuambia kuhusu ratiba hiyo kua: “Kituo kinatoa huduma kwa jamii ya wairaq kwa ujumla na kwa wakazi wa Karbala kwa namna ya pekee, baada ya jamii kufika kiwango cha juu cha mpasuko wa kifamilia, kimesha tatua makumi ya matatizo ya kifamilia yaliyo kua katika hatua tofauti, ratiba hii tuliyo andaa ya kundi la watoto hawa ni moja ya sehemu za shughuli zetu, tunatarajia kuwarudisha katika familia zao waendelee na maisha kama kawaida, kupitia utaratibu maalum unao endana na shughuli hiyo”.

Akaongeza kua: “Ratiba inalenga kutoa msaada wa kinafsi na kimaana, na inahusu makundi matatu, kundi la kwanza ni familia, la pili ni watoto –wakike na wakiume- na la tatu ni vijana, kupitia ratiba hiyo katika kila kundi tumejaribu kuweka utaratibu wa kubaini kila tatizo na kutafuta njia za kulitatua, tutaendelea na ratiba hii hadi tupate mafanikio tunayo tarajia”.

Kumbuka kua kituo cha utamaduni wa familia kimejikita katika mambo ya familia na jamii, kipo katika mkoa wa Karbala/ mtaa wa Mulhaq/ barabara ya Hospitali ya Hussein (a.s)/ ndani ya jengo la kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s). Kwa maelezo zaidi piga namba ya simu ifuatayo: (07828884555).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: